Hutakiwi kushangaa siku ukisikia lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond
kuwa ipo juu zaidi ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, hiyo ni
kutokada na mikakati pamoja na jitihada zinazozidi kuwekwa na uongozi wa
lebo hiyo.
Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne akiwemo Diamond,
Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na taarifa za chini chini
kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa chini ya lebo hiyo huku
bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na tayari amesharekodi
wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika Kusini. Lakini pia nje ya
kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya Diamond ni biashara kubwa
ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa kila siku.
Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.
Ukubwa wa jina la Diamond
Hili halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii
wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho
ni kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na
kazi zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection
wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika
endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi
kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa
Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia
Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.
Mashabiki wanaomsupport Diamond
Diamond ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo tayari
kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na maneno
kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza kutumia
pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya sasa kwa
Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.
Menejimenti ya WCB
Uongozi wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa
kufaulu kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya
na hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza
wakaifanya lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka
kufika huko.
Source:Bongo5
Monday, May 30, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment