Wikiendi hii mrembo huyo alizindua huduma yake aliyoipa jina ‘Wema Sepetu Mobile Application’ itakayowawezesha mashabiki wake kuwa naye karibu zaidi. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Kupitia Instagram, Wema ameandika:
Kwanza Kabisa nichukue nafasi hii Kusema Asante Mungu wangu kwa kunifanikisha kukamilisha kile ambacho nimekuwa nikikitamani na ambacho nimefanyia kazi kwa takribani ya miezi Mitano mpaka kufika siku hii ya leo… Lakini pia niseme Asante kwa Familia yangu yote kwa ujumla, Bila kusahau mashabiki wangu wapenzi kwa kunipa moyo wa kutokukata tamaa japokuwa kuna mengi ambayo kwa binadamu wa kawaida huwezi vumilia Ila kiukweli mashabiki wangu mmekuwa mnanipa nguvu na Courage everyday
Najisikia Fahari sana Leo hii kuwa Mwanamke wa Kwanza Barani Africa Kuwa na MobileApp inayonitangaza mimi Mwenyewe kama Content…. Kwa kutumia hii App unaweza kupata chance ya kupata zile habari zote za uhakika kuhusu Wema Sepetu… Kuna vingi ambavyo pia unaweza kupata kama Video Clips, Audio na Pictures kwa wale watumiaji wa Smart Phone… Lakini pia kwa wale wasio na Smart phone basi unapata Habari na Matukio mbali mbali kuhusu mimi ambayo sio Longo longo… Trust me with this app kuna mengi saaana mtakayoyapata… Ni Rahisi sana Una tuma Neno “Wema” kwenda namba 15404 and u are done…. Asanteni sana…. Nawapenda Mno… Huduma hii ipo Applicable kwa Mitandao Yote Tanzania…. What are u waiting for…?”
No comments:
Post a Comment