Wizkid tayari anaishi ile ndoto ambayo wasanii wengi wa Afrika bado
wanaiota. Kutoka kushirikishwa kwenye wimbo wa Drake ‘One Dance’ uliopo
kwenye album Views na ulioshika namba moja kwenye chart za Billboard
100, hadi sasa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaomsindikiza
Chris Brown kwenye ziara yake ya ‘One Hell of A Nite Tour’ barani
Ulaya.
Taarifa hiyo ilitolewa na Chris Brown mwenyewe kwenye akaunti yake ya
Instagram kabla ya Wizkid naye kuandika: 5th – 11th June I’ll be
supporting my brother @chrisbrownofficial !! Get ur tickets!!
#Onehellofanitetour Bringing the African wave!!”
Wizkid ana wimbo aliomshirikisha muimbaji huyo wa Marekani mwenye mashabiki wengi.
Monday, May 30, 2016
Wizkid Apewa Shavu Na Chris Brown, Amuongeza Kwenye ‘One Hell of A Nite Tour’ Ulaya
Labels:
Chris Brown,
Entertainment,
Wizkid
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment