Kama ulikuwa unasubiria kuona mashindano ya Big Brother Africa basi pole sana sababu kwa mwaka huu hayatakuwepo.
Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na
kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Afrila, huku
Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.
Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net
wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano
hayo hapo mwakani.
“We wish to thank Big Brother Africa fans far and wide for their
continues support over the past edition and promise that the shw will go
on, on Dstv, with new and excting productions in store from M-Net,”
wamesema.
Mpaka sasa taji hilo la Big Brother linashikiliwa na Idris Sultani
aliyefanikiwa kushinda mwaka jana na kupata zawadi ya fedha kiasi cha
dola laki tatu.
Sunday, May 22, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment