Huu ni mwaka wa Alikiba. Baada ya kusaini
mkataba mnono na Sony Music itakayomshuhudia akienda rasmi kimataifa,
staa huyo amepewa dili jingine la kufanya kazi na taasisi ya Jamie Oliver Food Foundation.
Trace Urban wameshare habari hiyo kwenye
Twitter. “This is .@OfficialAlikiba’s year! He has a dope partnership
w/the #JamieOliverFoundation too.”
Taasisi hiyo ya kimataifa inajihusisha na
masuala ya chakula na upishi. “Access to good, fresh, real food and the
basic skills to cook it has the power to transform lives, and that is
what the Jamie Oliver Food Foundation is all about,” imeandika kwenye
tovuti yake.
Taasisi hiyo inafanya kazi Uingereza,
Marekani Australia na hutoa mafunzo mbalimbali kuhusu chakula. “Our food
education programmes in schools, communities and with groups of
vulnerable young adults teach people about food, where it comes from,
how it affects their bodies and how to cook it.”
Taasisi hiyo ilianzishwa na mpishi maarufu wa Uingereza, James Trevor Oliver
Katika hatua nyingine mkataba wa Alikiba
na Sony utamwezesha kufanya collabo na msanii wa Marekani aliye chini ya
label hiyo pia.
“@SonyMusicAfrica will have USA/East Africa collaboration for@OfficialAlikiba with other #Sony artists,” wametweet Trace.
Habari hii kutoka http://www.bongo5.com
No comments:
Post a Comment