Series ya taarifa kubwa za michongo ya kimataifa aliyopata Alikiba mwezi huu imeendelea.
Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye,
Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa
jina ‘Alikiba TV.’
Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri
na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe
ufafanuzi zaidi.
“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake –
matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube
channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza
na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.
“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.
Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine
vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo
vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel
yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.
Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label
maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje,
amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita
‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.
Monday, May 30, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment