Diamond Platnumz alimpeleka Rich Mavoko kwenda kushoot video ya wimbo
wake mpya na wa kwanza akiwa chini ya Wasafi Records, imebainika.
Mavoko anadaiwa kuwa ameshasaini kuwa chini ya record label hiyo
inayokua kwa kasi kitambo tu lakini uongozi unasubiri hadi video yake
itakapokamilika ndipo atambulishwe rasmi.
Diamond na Mavoko walienda Afrika Kusini May 16 na ofcourse
hawakusema chochote zaidi ya muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ kuweka
picha hiyo juu akiwa kwenye ndege na kuandika: On Another Move…. Eeh
Mwenyez Mungu nibarikie na Hii…. pray #WcbWasafi.”
Mavoko anakuwa msanii wa tatu kuwa chini ya WCB baada ya Harmonize na Raymond.
-Bongo5
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment