Friday, May 20, 2016

Nay wa Mitego: Gigy Money Anatafuta Kiki Kwangu

MKALI wa Ngoma ya Saka Hela, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameamua kumfungukia muuza nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuwa anatafuta kiki kutumia jina lake katika mahojiano anayofanya na vyombo mbalimbali vya habari.

Akichonga na Showbiz Xtra, Nay alisema kuwa amekuwa akisikia juu ya Gigy akimsema si chochote kwake na kwamba ni mbahili alishawahi kumlipa elfu ishirini baada ya kumaliza kutengeneza video zake.


 “Yaani huyo Gigy anatafuta kiki, namshangaa sana kila sehemu kunisema hovyo, kwanza hatuendani kwa chochote,” alisema Nay.

Hivi karibuni katika mahojiano na Global TV Online, Gigy alisikika akimponda Nay kuwa ni mtu bahili na haitakuja kutokea yupo naye iwe kikazi ama vyovyote kwa kuwa hana hadhi ya kuwa naye.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.