Nchini Ujerumani wametengeneza Ndege aina ya LILIUM
kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yenye siti mbili, shepu ya yai na
inatumia umeme, imetengenezwa na mainjinia wanne wakijerumani wakidai
kuwa ndege hiyo yenye kupunguza matumizi na kurahisisha usafiri kwa
watu.
Ndege hii
inasemekana kuwa na uwezo wa kwenda hadi spidi ya kilometa 400 kwa saa,
kutumika kwenye eneo tambarare, kupaa na kutua kwa mita 15. Kingine
kikubwa ni kwamba inatumia umeme na inachajiwa kama simu pia
haina kelele pia ni kwa ajili matumizi ya mchana tu kwenye hali ya hewa
tulivu na sio usiku.
Mmoja wa msaidizi wa mmiliki wa ndege hiyo, Daniel weigand amesema wana mpango wa kuiingiza sokoni mwaka 2018, ameyazungumza haya …………
>>>”tunataka
ndege isiyo na gharama kubwa wala isiyokuwa na tatizo la utumiaji wa
miundombinu yake, pia iweze kutumika na watu wengi wenye uwezo wowote
ule sio watu wenye uwezo mkubwa tu ndo waweze kununua ndege hii”.
MillardAyo.Com
No comments:
Post a Comment