Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, amewataka wasanii wenzake kukaa mbali na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Rappa huyo ambaye alikaa rehab kwa muda mrefu ili kusaidiwa kuacha
matumizi ya Madawa ya kulevya, ameiambia Bongo5 kuwa matumizi ya Madawa
ya kulevya yamesabisha apoteze dira ya maisha yake.
“Kusema kweli Madawa ya kulevya yamenirudisha nyuma sana, sitaki kuzungumza mengi nadhani hilo liko wazi,” alisema Ibra.
“Mimi sikuwa hivi, niweyumba sana, ndio maana napenda kusema kila
kitu kwenye maisha kinatokea kwa sababu, na wenzangu wajifunze kupitia
mimi, na kwa wale wenzangu ambao walikubwa na matatizo kama yangu,”
aliongeza.
Ibra amesema kwa sasa ameacha kabisa matumizi ya Madawa ya kulevya huku akidai sasa hivi anatumia pombe na sigara tu.
Monday, May 30, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment