STORI: HAMIDA HASSAN WIKIENDA
Dar es Salaam: Huku kukiwa na
madai mazito ya kumchuna aliyekuwa mumewe ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mbunge wa Jimbo la
Donge, Zanzibar, Sadifa Khamis Juma, staa wa sinema za Kibongo, Wastara
sasa anaripotiwa kununua mjengo wenye gharama ya Sh. milioni 180 za
Kitanzania, Wikienda limechimba.
Pamoja na misukosuko yake na Sadifa,
ubuyu kutoka kwa mtu wa karibu wa Wastara unanyetisha kuwa Wastara kwa
sasa mambo yake ‘supa siyo dizeli’ kwani anaonekana mshiko umemtembelea
na kununua nyumba hiyo iliyopo Gongo la Mboto, Dar.
“Jamani nawapa ishu lakini msinitaje, lakini ukweli ni kwamba Wastara amenunua nyumba maeneo ya Gongo la Mboto.
“Wapo wanaosema eti mbwembwe zote
anazifanya na fedha alizomchuna Sadifa lakini pia wapo wanaosema kuwa
nyumba hiyo amepangishiwa na aliyekuwa mpenzi wake, Bond Bin Sanan kwani
maeneo aliyonunua nyumba hiyo ndiyo anayokaa Bond,” alifunguka
‘kikulacho’ huyo.
Sosi huyo aliendelea kunyetisha kuwa,
pamoja na kwamba Wastara kwa sasa yupo nchini Msumbiji kibiashara
(anafanya biashara ya nguo) lakini nyumba hiyo wanakaa watoto wake.
Baada ya habari hiyo kutua kwenye meza ya Wikienda, mwanahabari
wetu alimtafuta Wastara kwa njia ya simu baada ya kuhakikishiwa kuwa
hayupo Bongo, alipopatikana alikiri kununua nyumba kwa Sh. milioni 180.
Katika mahojiano ya Wikienda na Wastara, mambo yalikuwa hivi;
Wikienda: Wastara kuna madai kuwa umepangishiwa nyumba na Bond kwa sababu mmerudiana ingawa wapo wanaosema umeinunua, je, hilo likoje?
Wastara: Unajua watu
wanapenda kunizushia lakini mimi sipendi. Huyo Bond sijarudiana naye
bali ninaongea naye kwa sababu ya kazi (uigizaji). Kuhusu nyumba
nimenunua mwenyewe.
Wikienda: Kuna madai mengine kuwa fedha ulizonunulia nyumba ulimchuna mbunge (Sadifa), wewe unasemaje?
Wastara: Kwanza mimi
sikuona fedha ya kumchuna huyo mbunge na hakuna fedha aliyonipa. Mimi ni
mfanyabiashara, biashara zangu za madini, nguo na urembo ndizo
zinaniingizia fedha. Ifahamike kuwa nilianza kufanya biashara tangu
kitambo.
Wikienda: Je, ni kweli umeuza nyumba yako ya Tabata? Au ni kwa sababu inatakiwa ibomolewe hivyo umeisusa?
Wastara: Sijaiuza, naikarabati, Mungu akipenda nitawaweka watoto yatima kwani ndiyo mipango yangu ya siku nyingi.
Sadifa alipotafutwa kwa njia simu ili kusikia kauli yake, hakuweza kupatikana hewani jitihada zinaendelea.
No comments:
Post a Comment