DAR ES SALAAM: Ubuyu wa motomoto wa mjini ni kwamba, zile mbwembwe zote
za penzi la mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris
Sultan, zinadaiwa kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema,
Idris wamwagana rasmi.
Wikienda limeng’atwa sikio kuwa, kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’
kwenye ile Pati ya Black Tie iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King
Solomoni pale Namanga, Dar ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana
kitambo.
Hata hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye
zilivunjwa picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele
ili kuua soo.
wema-na-idriss-insta Sasa ubuyu ulionyooka kutoka kwa chanzo cha
kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao unadai kwamba,
kilichotokea kwenye pati hiyo zilikuwa ni mbwembe za kuzuga zilizotokana
na huruma ya Idris.
Ilidaiwa kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu
ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni
kwamba mambo yalishaharibika.
wema na idris 2“Unajua watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris
walishaachana kitambo na pale (King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo
tu, japokuwa haijulikani moja kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini
Wema anadaiwa kuwa tatizo kwa Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya
kila kukicha,” alitonya sosi huyo.
Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu kinaendelea, wana-ubuyu
wetu walifuatilia akaunti zote za mastaa hao katika mitandao ya kijamii
kuona kama mbwembwe zao zinaendelea na kubaini kuwa hawako sawa baada ya
kusoma ujumbe wa Wema unaoonesha kumbembeleza Idris huku jamaa huyo
akionesha wazi kuwa hakuna mapenzi bali ni drama tu.
Ili kuleta ushahidi, tunakukaribisha hapa kusoma nukuu zao mtandaoni;
MANENO YA WEMA
“Having you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to
cry on every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I
wouldn’t want to lose this feeling over anything…
“I realized without u then i ain’t complete…. You have stood by me in
good times and bad and even when i messed up so bad you would look me in
the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gona fix this”…
“Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing i want
on this earth… I will love you until forever, until death do us part we
will be together…
“I will hold on to you till da last minute because together we will get
there…. I love you with my life…. For I believe you are my true love, my
baby and inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia
kuandika Wema akimlilia Idris.
IDRIS NAYE ALIANDIKA:
“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”
WEMA ASAKWA
Wikienda halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa,
alipopigiwa simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia
hakuujibu.
Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.
UBUYU WAKAMILIKA KWA IDRIS MWENYEWE
Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila kuacha lolote.
Kwa mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.
“Mimi nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani
ndiyo kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka
kwenye matangazo. Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia
shoo lakini mimi nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,”
alifunguka Idris.
Idris alienda mbali zaidi na kusema kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine
anayempenda na siku si nyingi mambo yakikaa sawa, atamuanika.
“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,” alisema Idris.
WEMA NA IDRIS
Awali Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua
kujiachia ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa
bahati mbaya ukachoropoka.
Source:Global Publishers
Monday, July 18, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment