Friday, July 1, 2016

Ni Kosa Kubwa Sana Kumfananisha Rais Magufuli na Dikteta

Kuna mawili, either watu hawajui maana na dhana nzima ya udikteta ama kwa makusudi wameamua kupotosha jamii. Viongozi mbalimbali hasa wa upinzani wamesikika wakimwita Magufuli kama Rais dikteta. sio kweli hata kidogo..

Nini Maana ya Dikteta?, Dikteta ni aina ya utawala wenye kutoa amri kama Imla. Ni neno la kumtaja mtawala asiyebanwa na sheria na hutumia nguvu ya dola kuendeleza utawala wake na kutokubali upinzani.... Kama Magufuli asingekubali upinzani si angefuta vyama vya siasa?. Ni marangapi kapokea mawazo wa wapinzani? (rejea alivyotembelewa na Maalim Seif na Prof. Lipumba ambao ni wapinzani)..

Sifa Kuu za Dikteta...
1, Mtu anayeshika mamlaka yote mikononi mwake.... Tokea lini Rais kashika mamlaka yote mikononi, je mawaziri wanaotumbua, wakuu wa mikoa wanaotumbua, wakuu wa wilaya wanaotumbua, PM anavyotumbua ushasikia wameingiliwa na Rais?... Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe. Magufuli yupo kwa ajili ya sisi wanyonge...

2. Hakubali Uchaguzi wa kisiasa au anahakikisha uchaguzi si huru...Magufuli huyu alibariki uchaguzi wa meya wa Dar es Salaam kufanyika na Ukawa wakashinda, angekuwa dikteta angebariki au kukubali uchaguzi huo?. Juzi na jana Ukawa walifurahi baada ya wagombea wao kushinda nafasi ya wenyeviti vya vijiji huko Geita, mbona huyo mnayemwita dikteta kakubali matokea?.....

3. Haheshimu haki za binadamu...... Hii ni moja ya sifa ya Rais dikteta... Wananchi tunashangaa kuona wapinzani wanamwita Magufuli ni dikteta. ni wazi hakuna mtu anayeheshimu haki za binadamu hasa wanyonge kama Rais Magufuli. kila speech anayotoa ni kulilia wanyonge, kila tukio anapoenda Magufuli ulilia wanyonge sasa kama haheshimu haki za binadamu angelilia wanyonge?

4. Anatoa amri kama sheria... Ni lini Rais Magufuli katoa amri bila kufata sheria?. Mara zote Magufuli amekuwa akifanya maamuzi kwa kufata katiba, sheria zilizopo nchini..... na sheria (bill) wabunge ndio walizitunga ambapo ndani ya bunge wapo wabunge wa upinzani... Tuacheni Rais Magufuli apige kazi..

5. Bunge na mahakama kufata maagizo yake..... Moja ya jambo tunalolivunia kama taifa ni uhuru wa bunge na uhuru wa mahakama. kama bunge lingekuwa linafata maagizo yake mbona inatokea kipindi wapinzani wanashinda kwa hoja (rejea 5 years Plan, ambapo Mwanasheria Mkuu alichemsha). Bunge hili limeonyesha liko huru, tena sana. kinachotokea ni ukomavu na ushupavu wa Dr. Tulia kama kiongozi wa bunge... Mahakama pia ziko huru, na ndio maana tumeona hata wapinzani wakishinda katika kesi mbalimbali za uchaguzi zinazowakumba... na hata kitendo cha wapinzani kukimbilia mahakamani pale wanapobanwa ni kiashiria tosha kuwa mahakama ni huru na Rais au serikali haiingilii mahakama...

NB: Hivyo ni kosa kubwa sana, tena sana kumlinganisha, kumfananisha au hata kujaribu kumfananisha Rais Magufuli na watu kama Adolf Hitler, Benito Mussolin, Mao Zedong, Augusto Pinochet, Pol Pot, Idi Amin au Sani Abacha.......

Magufuli kaamua kwa dhati kabisa kutumikia wanyonge. kaamua kwa dhati kabisa kuwa mzalendo kwa kuwapigania na kupigania haki za wanyonge. hivyo tumuache apige kazi... tusubiri 2020 muda wa siasa....

Imeandikwa na Pagan Amum/JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.