Monday, July 4, 2016

Darasa Afunguka Kuhusu Ishu ya Linah Kutamani Kuwa Naye, Adai ‘Nina Mpenzi’


Mkali wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na kutamani kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu.
Akizungumza na Wikienda alipotembelea Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia ujasiri kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu na wanaaminiana.
“Namshukuru kwa kunikubali, kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.
Darasa alifunguka hayo baada ya hivi karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.
Share na Marafiki:

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.