Friday, July 1, 2016

Ureno Yachapa Mtu Robo Fainali ya Euro

ureno
ureno
Ureno imetinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa na kuwa nchi ya kwanza kufuzu katika hatua hiyo baada ya kuwafunga Poland kwa mikwaju ya penalti 5-3.
Dakika 120 zilishuhudia mchezo huo ukiisha kwa suluhu ya goli 1-1.Robert Lewandowski aliiandikia goli Poland mapema kipindi cha kwanza katika dakika ya tatu ya mchezo kabla ya Renato Sanches kuisawazishia timu yake ya Ureno.
Ricardo Quaresma alikuwa shujaa kwa timu yake baada ya kupiga penalti ya mwisho iliyoivusha katika hatua nyingine huku kiungo wa Jakub Blaszczykowski akikosa mkwaju wa penalti kwa upande wa Poland.
Ureno itakutana katika hatua ya nusu fainali na mshindi wa mchezo kati ya Wales na Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.