Monday, July 18, 2016

Makonda Akanusha Wasio Na Kazi Kukamatwa







Kumekuwepo na taarifa ambazo zimekuwa zikisambaa na zimekuwa zikimnukuu Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuwa ametoa agizo la kufanyika ukaguzi kwa kila nyumba na ambao watakutwa hawana shughuli maalum basi wakamatwA Akizungumza katika kipindi cha Power Breakfast kinachoruka kupitia Clouds Fm, Makonda amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa jambo hilo halina ukweli wowote na kinachofanyika ni baadhi ya watu kusambaza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii.
“Sasa tuwakamate wote tunawapeleka kwenye magereza gani?, hilo jambo halipo hivyo, sisi tunataka kuwafahamu watu wetu ili hata linapokuja jambo la maendeleo tujue tunaenda kuwapa watu sahihi,
“Mfano kwa sasa tuna mpango wa kuchukua vijana 1,200 tuwapeleke katika mafunzo ya ufundi na ujasiriamali kwa miezi mitatu sasa kama hatuwatambui tutawapa nafasi watu wengine ambao sio wa Dar lakini tukiwafahamu inakuwa rahisi,” alisem Makonda.
Aidha Makonda amekanusha kuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii ambazo zinaanza na neno la RC au DC hivyo kuwataka watumiaji wa mitandao kuwa makini na watu hao.
“Mimi JamiiForum, Facebook na Instagram natumia jina moja la Paul Makonda sina jina tofauti na hilo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.