Baada ya mtangazaji wa Clouds FM, Diva kudai kwamba hamjui msanii wa
muziki Ruby, Ruby ameendelea kutema cheche kuhusiana na kauli hiyo.
Muimbaji huyo ambaye ameachana na uongozi wake wa zamani wa THT,
ameonyesha kuchukizwa na kauli hiyo ya Diva na kila akiulizwa kuhusu
kauli hiyo amekuwa akitoa maneno makali.
“Kuhusu Diva, bora tu niachane naye maana sioni vitu vya kumuongelea
kama anavyofanya yeye,” Ruby aliliambia gazeti la Mtanzania “Zaidi
namuonea huruma tu, namsikitikia na ninamwombea kwa Mungu amrudishie
akili zake. Nahisi ana ugonjwa wa kusahau, jambo ambalo ni baya sana
kulingana na umri wake,”
Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa amefunga ukurasa wa kuzungumzia
masuala ya uongozi wake uliopita kuhu akidai kwa sasa ana nafasi ya
kufanya vizuri zaidi kimuziki.
Monday, September 19, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment