Msanii mkongwe na asiyesahaulika katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya
dudu baya amekivua nguo kituo cha clouds fm kwa kuwaita ni wanafki
wakubwa, wanyonyaji wa wasanii, na wenye kuharibia wasanii ndoto za
mziki wao
Mamba alitolea mfano wasanii wanazungushwa mikoani kwenye tamasha la
fiesta na kuambulia ujira mdogo, huku akisema pesa wanayopata kwenye
hilo tamasha huishia hukohuko mikoani na hurudi dar wakiwa wamepayuka
hawana kitu mfukoni
Dudu alisema hayo akipokuwa kwenye kipindi cha usiku cha FRIDAY NIGHT LIVE... FNL kinachorushwa na EATV
Alienda mbali zaidi kwa kumpongeza msanii mwenye kipaji anayekuja juu
ruby kwa kusema ametoka kwenye minyororo ya wafu FM akawasihi na wasanii
wengine wamuige ruby kwani ameonesha mfano
Akionekana mwenye afya km alivyokuwa zamani, amesema wafu fm hawajapiga
nyimbo zangu kwa miaka sita sasa lakini sijatetereka naendelea na maisha
yangu kama kawaida
Wakati akiendelea kuwatolea uvivu clouds fm mtangazaji wa kipindi hicho
sam misago alitumia mbinu ya ziada kumtoa kwenye kile akichokuwa nacho
moyoni
Hata hivyo alipongeza redio ambazo zipo chini ya IPP km East africa
radio, radio one, capital fm na kusema hajawahi kuombwa pesa na
mtangazaji au dj yeyote wa kituo hicho ili wimbo wake uchezwe hewan
Amevitaka vituo vingine kuiga vyombo vya ipp media
Kwa maneno ya dudu baya ni dhahiri wasanii wengi ni watumwa wa baadhi ya media house
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment