Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds Media Group, Ruge Mutahaba
amesema yeye ni mtu ambaye anaongoza kwa kutukanwa katika tasnia ya
muziki kutokana na harakati zake za kuupigania muziki.
Akiongea Ijumaa hii katika semina ya wasanii wachanga wa Dodoma
iliyofanyika katika Ukumbi wa Royal Village, Ruge amewataka wasanii hao
kuacha kukata tamaa katika harakati wanazopitia.
“Mimi ni mtu ninaeongoza kwa kutukanwa kwenye tasnia ya muziki,” alisema
Ruge. “Nimetukanwa sana lakini hilo haliniumizi, najivunia kwa kuwa
tumepambana sana kuusimamisha muziki wetu hadi kufika hapa,”.
Ruge Mutahaba ni mmoja kati ya watu waliosaidia kwa namna moja kuchochea
kukuwa kwa muziki wa bongofleva nchini licha ya baadhi ya watu
kutokubali harakati zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment