Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa
wakifanya kazi na Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The
Industry baada ya kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.
Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni mshkaji
wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana
kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua
kubadilisha ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.
“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You, naweza
kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,” Jux
ameimbia Bongo5.
“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi kuwasema
sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo
baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda
nisingepata kitu tofauti,” amesisitiza.
Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China na pia
Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika
Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.
“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya naye kazi
pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi haijaniathiri
chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka kufanya,
kwahiyo mimi naona ni sawa. Kwanza mimi ni mmoja wa watu niliyeona hivyo
yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia kwasababu alikuwa
anafanya kazi sana.”
Wiki iliyopita Jux aliachia wimbo wake mpya, Wivu aliorekodi kwenye studio za AM Records.
Bongo5
Monday, July 18, 2016
Nahreel Alinitengenezea Hit Yangu ya Kwanza Afrika, Siwezi Kuacha Kufanya Naye kazi – Jux
Labels:
Entertainment,
Jux,
Nahreel
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment