MKALI
wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ anadaiwa kunasa ‘kimalovee’ na
msanii mwenzake, Jamila Abdallah ‘Baby J’ ambaye muda mwingi makazi yake
ni Zanzibar, lakini mara kwa mara wamekuwa wakionekana kujiachia maeneo
mbalimbali ya Jiji la Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo
karibu na wasanii hao kilieleza kuwa, hiyo ndiyo kapo mpya ya mjini
licha ya kuwa, hawajaamua kuweka wazi uhusiano wao kwa mashabiki lakini
si siri tena sababu hata wasanii wenzao wengi wanafahamu.
Jamila Abdallah ‘Baby J’
Baada ya kuupata ubuyu huo, mtandao wa Global Publishers
ilimvutia waya Baby J ambaye aliruka vikali na kudai ni mtu wake wa
karibu tu, upande wa pili Mo Music alipotafutwa alianza kwa kuangua
kicheko na kusema kuwa;
“Kweli mjini mtu hakunyimi umbeya sijui mmeyapataje haya, sioni cha ajabu hapo ila muda ukiwadia nitaweka wazi kila kitu.”
No comments:
Post a Comment