Kuna vita vikali vya maneno kati ya TID na aliyekuwa kijana wake, Billnass.
Katika mahojiano mengi aliyofanya, Mnyama anaonekana kukerwa na kitendo cha rapper huyo wa Chafu Pozi kuondoka kinyemela Radar Entertainment – label iliyomtoa. Anaamini kuwa Bill ni mtu mwenye tamaa na hayupo real na kwamba alimtumia tu kupata jina na baada ya kufanikiwa kamtema kama ganda mua!
Hata hivyo Bill ambaye jina lake halisi ni William, haoneshi kutaka kumjibu TID, hataki makuu na ‘anaplay smart.’
“Kuna vitu vingi sana ila mimi sitaki kuzungumza sana, ninachoweza kusema ni kuwa nampenda TID na namheshimu,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Bill bado anasisitiza kuwa mkataba wake, hata kama ulikuwa wa maneno ulimalizika baada ya mwaka mmoja na alikuwa huru kwenda popote. Anasema hawezi kuongea na TID moja kwa moja lakini ameshaongeza na watu anaowaheshimu ili waongee na bosi wake huyo wa zamani ili wayaache yaliyopita yapite na wasichafuliane kwenye vyombo vya habari.
Msikiliza hapo chini.
No comments:
Post a Comment