Rapper kutoka Kenya Prezzo hatimaye amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Michelle Oyola ambaye amekuwa naye karibu sana siku za hivi karibuni.
Prezzo ambaye pia kipindi cha nyuma aliwahi kuwavisha pete wanawake wawili wa kwanza akiwa ni mama mtoto wake Daisy na marehemu Goldie. Taarifa hii imekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya ambapo wengi wanaamini kuwa huyu ndiye atakuwa mke wa Prezzo.
Kupitia mtandao wa Instagram Prezzo aliweka picha iliyoambatana na ujumbe: That rock on her finger’s like a tumor, her hand ain’t gon fit in her purse #MrsMakini #Rapcellency #GodsSon.”
No comments:
Post a Comment