Lakini imetokea kwa msanii wa PKP, Nedy Music ambaye video ya wimbo wake Usiende Mbali aliomshirikisha bosi wake Ommy Dimpoz imefikia mafanikio hayo.
“1 MILLION VIEWS 1000000+… Ndani ya Siku 13,” ameandika Nedy kwenye Instagram kusherehekea matunda hayo.
“Shukrani za dhati ziende kwa mungu mwenyezi tangia nlipotoka mpka sasa nilipo, pili kwa management yangu nzima ya PKP,” ameongeza.
“Tatu sitoacha kushukuru na kusema ya moyoni kwa wadau wote ambao wanasapoti kazi za kijana wenu tangia nimeanza mpaka sasa siku hadi siku, Ahsanteni sana na sitawaangusha. #USIENDEMBALI BY @NEDYMUSIC FT @OMMYDIMPOZ . Mungu awe nanyi nawapenda sana sana.”
No comments:
Post a Comment