Saturday, May 21, 2016

Nisher Aingia Kwenye Ugomvi na G Nako baada ya kuipotezea video yake ya ‘Arosto’ na kuirudia na Hanscana, Ishu Nzima Ipo Hapa

Muongozaji maarufu wa video Tanzania, Nisher ameamua kutoa dukuduku lake baada ya G nako kuipotezea video aliyoitengeneza yeye ya ‘Arosto’ na kwenda kuirudia na director mwingine.

Nisher mfululizo wa video nyingi aliyoweka Instagram Nisher alikuwa analalamika kuwa G nako na Weusi walimwambia video hiyo haiwezi kutoka kwasababu ilikuwa haijafikia viwango walivyokuwa wanataka, lakini cha kushangaza hata alipotaka kuirudia walisema hawana pesa japo yeye aligharamikia video hiyo ya kwanza.

“Huu ni Usaliti! Nataka pesa zangu zirudi Kistaarabu tu. Haya ni maisha na maisha lazima yaendelee” Nisher ameandika kwenye Instagram yake na kuelezea kuwa hawezi umia kwasababu hakuigharamikia video hiyo.

A video posted by NISHER (@nisherx) on

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.