Monday, May 30, 2016

Maneno Ya kumkejeli Wema Sepetu Yamtokea Puani Harmonize


Harmonize amelazimika kuamka na hangover ya matusi kutoka kwa mashabiki wa Wema Sepetu baada ya kusambaa video inayomuonesha akiwa na washkaji zake akishuka mistari ya hip hop inayoishia kumkejeli ex wa bosi wake, Sepetunga.
HARM
“Nasikiaga uzuri wa nyumba usikufanye utembee peku, sista duu usitoe mimba kesho ulie kama Wema Sepetu,” anaonekana Harmonize akirap na kushangiliwa na washkaji zake. Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Wema waliomporomoshea matusi usiku kucha kuanzia jana.
Wema aliupata ujumbe huo na aliamua kuujibu kwa busara zaidi kwa kuweka nukuu ya Angelina Jolie kwenye picha hiyo chini na kuandika tu: Well. Arent you??”
13151360_1072023689554363_894032107_n
Mpenzi wake Idris alijibu pia lakini kama kawaida kwa utani mwingi.
“As i sit here nikakumbuka kitu “Jamani nimeanzisha format yenye ustaarabu na taratibu, kwa yoyote anayetamani kutafuta kiki kupitia mimi kuna contract nimeandaa ni makubaliano mimi na wewe kwa percent ya mapato utakayopata kwa kiki hiyo ili itunufaishe wote tena ntakupa hadi na idea za jinsi ya kunitukana na kunimaliza kwasababu najua mwisho wa siku tunavuta mpunga wetu wanashangaa kesho mi na wewe tunacheka tu” hii naiita #MoneyKick #KikiPesa clients wote email me bei ni maelewano,” aliandika.
Katika kujaribu kuliua soo, Harmonize alijirekodi voice note na kuituma kwa makundi ya WhatsApp ya WCB lakini snitch mmoja aliivujisha na kuiweka Instagram. Kwenye sauti hiyo Harmonize anasikika anasema kuwa siku wanarekodi video hiyo aliomba isisambae kwakuwa aliamini ingekuja kumletea matatizo.
“Bahati mbaya imetokea hatujui nani amevujisha video imeleak,” anasema. Anadai kuwa mkakati waliojadili kufanya ni kuipigia promo ngoma mpya ya Raymond ‘Natafuta Kiki’ ili kumaliza nguvu ya video hiyo.
Kitu anachotakiwa kukifahamu Harmonize sasa ni kuwa kile kinachojadiliwa kwenye magroup ya WhatsApp ya WCB hakibaki humo tu, kuna snitches kibao wanaoweza kuumwaga mchele kwa ndege wengi hasa wasiohusika!

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.