Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limempongeza Alikiba baada ya kusaini mkataba wa kimataifa na label kubwa duniani, Sony Music.
BASATA lilimpongeza Alikiba kupitia akaunti ya Twitter na kuelezea kuwa mafanikio hayo yamekuja kutokana na nidhamu aliyonayo.
“Tunampongeza Msanii Ali Kiba kwa kusaini mkataba na Kampuni ya Kimataifa ya Sony Music. Nidhamu, maadili & Sanaa ya staha hulipa,” waliandika BASATA
Alikiba naye aliwashukuru Basata kwa kuandika: Nalishukuru @BasataTanzania kwa pongezi kwani nyinyi ni Kama wazazi katika sanaa yetu Asanteni sana proudly TZ.”
No comments:
Post a Comment