Msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa Mitego ambaye alisumbua sana na
wimbo wake 'Shika adabu yako' ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa
(BASATA)
na sasa ameachia wimbo wake mpya 'Saka hela' amefunguka na kusema kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata au kushinda tuzo..
Nay wa Mitego aliyasema haya alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha
eNEWS na kuwataka mashabiki wa muziki wake watambue kuwa yeye hafanyi
muziki ili kupata tuzo au kushinda tuzo bali yeye anafanya muziki kutoa
burudani, kurekebisha sehemu anapoona si sawa pamoja na kumuingizia
kipato ndiyo maana siku zote huwa anajiita mwanamuziki mfanyabiashara.
"Mimi siku zote sifanyi muziki ili nipate tuzo au nishinde tuzo hata
mashabiki zangu naomba mtambue kuwa mimi sifanyi muziki kwa ajili ya
tuzo" alisema Nay wa Mitego.
Katika hatua nyingine Nay wa Mitego anadai kuwa anapotoa ngoma zake za
kuchana watu au kurekebisha baadhi ya mambo kwa watu au jamii huwa
zinapokelewa vizuri zaidi na kuleta changamoto kwenye muziki ikiwa
pamoja na kuchangamsha muziki wa bongo.
Saturday, May 21, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment