Monday, May 30, 2016

Zijue Faida/Hasara za Kurudiana Na Mpenzi Wako Wa Zamani

Kuna faida ya wapenzi kuachana na kurudiana? Vipi kuhusu hasara zake? Hiyo ndiyo mada yetu ya leo kama inavyojieleza. Bila shaka unawajua watu ambao walikuwa wakiishi pamoja kimapenzi, iwe ni ndoa, uchumba au uhusiano wa kawaida ambao wamewahi kutengana na baadaye wakarudiana, iwe ni mara moja au zaidi.
Yawezekana hata wewe ukawa miongoni mwa watu wa aina hiyo, kwamba uliwahi kutengana na mtu umpendaye lakini baadaye ukajikuta unarudiana naye na kuanzisha upya uhusiano.
Je, kuna faida na madhara gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi unawachukuliaje?

NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MAPENZI

Yawezekana aina hii ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya muda mkarudiana tena, likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi za Kiafrika lakini kwa taarifa yako, hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano wa kimapenzi duniani kote.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanandoa au watu ambao wapo kwenye uhusiano imara wa kimapenzi, wamewahi kupitia kipindi hiki kigumu cha kutengana na kurudiana, wengine wakifanya hivyo mara kadhaa.
Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kutengana, hushindwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao hata kama bado wanapendana kwa kuona jamii itawashangaa kuwaona wakiwa pamoja tena baada ya kuachana kwa kashfa na vurugu kubwa.
Kama na wewe ni miongoni mwa watu wa aina hii, narudia kukusisitiza kwamba hilo ni jambo la kawaida na linafanyika duniani kote.

MADHARA YAKE

Yapo madhara mengi yanayowakumba watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano. Inapotokea mmeachana na kila mmoja akaanzisha ukurasa mwingine wa mapenzi, lazima atakutana na mazingira tofauti kabisa na yale mliyozoea kuishi pamoja.
Endapo atakutana na mtu mwingine ambaye amekuzidi vitu vingi, hata ikitokea wakaachana na akarudi kwako, hawezi kukupenda kwa kiwango kile kama ilivyokuwa mwanzo kwa sababu tayari kuna vitu vipya vimeingia ndani ya kichwa chake na huo utakuwa ufa mwingine ambao hapo baadaye utasababisha muachane tena.
Upo ushahidi wa wapenzi ambao baada ya kutengana na watu waliokuwa wanawapenda mwanzo, walikutana na watu wengine wenye uwezo wa kuwaridhisha na kuwafurahisha faragha kuliko ilivyokuwa kwenye uhusiano uliovunjika. Inapotokea ukarudiana na mpenzi wa aina hii, ambaye tayari ameshauona ulimwengu mwingine wa kuridhishwa kimapenzi ambao kwako hakuwahi kuuona, kamwe hawezi kutulia na wewe. Hesabu maumivu.
Suala lingine ni maradhi. Katika dunia iliyochafuka kama hii tunayoishi, ni hatari kurudiana na mwenzi wako kwa sababu hujui baada ya kutengana na wewe alikuwa akitoka na nani. Ni rahisi kukuletea maradhi ya zinaa au Ukimwi hasa kama alikuwa anatoka na watu wasio sahihi. Unapaswa kuwa makini katika hili.
Kulipizana visasi ni tatizo lingine linaloweza kuwakumba watu wanaoishi kwenye uhusiano wa aina hii. Yawezekana wewe ndiye uliyemuumiza mwenzi wako wakati mnaachana, ukautesa moyo wake na kushindwa kumuonea huruma wakati akiteseka.
Inapotokea mmerudiana, wengi hubaki na vinyongo ndani ya mioyo yao na kwa sababu wewe ndiye uliyemuumiza na yeye atakutafutia sababu ya kulipa kisasi ili na wewe uhisi maumivu kama aliyoyahisi yeye wakati mnaachana.

FAIDA ZAKE

Narudia kusisitiza kwamba japokuwa wengi wanaona kama ni jambo la ajabu kurudiana na mtu uliyekuwa unampenda, ni jambo la kawaida kabisa na watu wengi wanafanya hivyo duniani kote.
Takwimu zikionesha kwamba wanandoa au wapenzi waliowahi kupitia kipindi cha kutengana kisha wakarudiana tena, wana nafasi kubwa ya kudumu kwenye uhusiano wao kwa kipindi kirefu zaidi.

Zifuatazo ni faida za kuachana na kurudiana.

TAYARI MNAJUANA: Mara nyingi unapoanzisha uhusiano mpya, unaweza kudhani kwamba unampenda sana mtu uliyenaye kwa sababu bado humfahamu kwa kina lakini ukishamjua kwa undani, hasa tabia zake, yale mapenzi uliyokuwa nayo huisha haraka kwa sababu ya upungufu utakaoubaini.
Unaporudiana na mwenzi wako, huanzi upya kwa sababu kama ni kumjua tayari unamjua na yeye anakujua, unaelewa udhaifu na uimara wake, hali kadhalika na yeye anakujua kwa hiyo mkiamua kuwa ‘serious’, kazi inakuwa nyepesi kuliko kuanza upya na mtu mwingine.
 
MMESHAKOMAA KIHISIA: Uamuzi wa kumrudia mtu aliyewahi kukuumiza, huhitajiujasiri mkubwa sana na ukiona umeweza kumsamehe na moyo wako bado unamhitaji, hiyo ni ishara ya ukomavu wa kihisia. Kama mkirudiana pamoja, hakuna tena jambo linaloweza kuwasumbua kwa sababu mmeshapitia milima na mabonde.
Kuna msemo mmoja maarufu kwamba huwezi kuona umuhimu wa kitu mpaka utakapokipoteza. Muda ambao mmeachana, kila mtu hupitia kipindi kigumu kihisia. Huu ndiyo muda ambao unaweza kupima kati ya mazuri na mabaya ya mwenzi wako, yapi yalikuwa mengi.
Ukiona moyo wako bado unamhitaji hata kama yapo aliyokukosea, tafsiri yake ni kwamba umeona umuhimu wake na utakapopata nafasi ya kurudiana naye utakuwa makini usimpoteze tena.
HISIA ZAKO ZIMETULIA: Inapotokea unakorofishana mara kwa mara na mwenzi wako, zile hisia tamu za mapenzi kati yenu hupotea kabisa na matokeo yake mnaishi kimazoea. Lakini inapotokea mmetengana na kila mmoja akaendeleana mambo yake, hisia hutulia na kurudi upya. Mnaporudiana kila mmoja anakuwa mpya kihisia hivyo mnakuwa na nafasi kubwa ya kudumu.
HAKUNA CHA KUWAYUMBISHA TENA: Wahenga wanasema nahodha mzuri wa meli hupimwa wakati bahari imechafuka. Ikiwa mmeshapitia kwenye machafuko makubwa yaliyosababisha mpaka mkaachana, wakati mwingine kwa vurugu kubwa, ni dhahiri kwamba kila mmoja ameshapata uzoefu.
Hata ikitokea mmekorofishana tena, hakuna atakayekuwa tayari kuona mnarudi kule mlikotoka hivyo mtamaliza vizuri tofauti zenu

Maneno Ya kumkejeli Wema Sepetu Yamtokea Puani Harmonize


Harmonize amelazimika kuamka na hangover ya matusi kutoka kwa mashabiki wa Wema Sepetu baada ya kusambaa video inayomuonesha akiwa na washkaji zake akishuka mistari ya hip hop inayoishia kumkejeli ex wa bosi wake, Sepetunga.
HARM
“Nasikiaga uzuri wa nyumba usikufanye utembee peku, sista duu usitoe mimba kesho ulie kama Wema Sepetu,” anaonekana Harmonize akirap na kushangiliwa na washkaji zake. Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Wema waliomporomoshea matusi usiku kucha kuanzia jana.
Wema aliupata ujumbe huo na aliamua kuujibu kwa busara zaidi kwa kuweka nukuu ya Angelina Jolie kwenye picha hiyo chini na kuandika tu: Well. Arent you??”
13151360_1072023689554363_894032107_n
Mpenzi wake Idris alijibu pia lakini kama kawaida kwa utani mwingi.
“As i sit here nikakumbuka kitu “Jamani nimeanzisha format yenye ustaarabu na taratibu, kwa yoyote anayetamani kutafuta kiki kupitia mimi kuna contract nimeandaa ni makubaliano mimi na wewe kwa percent ya mapato utakayopata kwa kiki hiyo ili itunufaishe wote tena ntakupa hadi na idea za jinsi ya kunitukana na kunimaliza kwasababu najua mwisho wa siku tunavuta mpunga wetu wanashangaa kesho mi na wewe tunacheka tu” hii naiita #MoneyKick #KikiPesa clients wote email me bei ni maelewano,” aliandika.
Katika kujaribu kuliua soo, Harmonize alijirekodi voice note na kuituma kwa makundi ya WhatsApp ya WCB lakini snitch mmoja aliivujisha na kuiweka Instagram. Kwenye sauti hiyo Harmonize anasikika anasema kuwa siku wanarekodi video hiyo aliomba isisambae kwakuwa aliamini ingekuja kumletea matatizo.
“Bahati mbaya imetokea hatujui nani amevujisha video imeleak,” anasema. Anadai kuwa mkakati waliojadili kufanya ni kuipigia promo ngoma mpya ya Raymond ‘Natafuta Kiki’ ili kumaliza nguvu ya video hiyo.
Kitu anachotakiwa kukifahamu Harmonize sasa ni kuwa kile kinachojadiliwa kwenye magroup ya WhatsApp ya WCB hakibaki humo tu, kuna snitches kibao wanaoweza kuumwaga mchele kwa ndege wengi hasa wasiohusika!
Audio | Raymond - Natafuta Kiki | Mp3 Download 

https://my.notjustok.com/track/download/id/95274/by/uV%7EMEAxr02

Download Audio | Kid Ink – Never Smoke

Audio | Kid Ink Never Smoke | Mp3 Download

Photos: Shilole Na Vanessa Walipokutana Kwenye Stage Usiku Wa May 29 2016 Club Billcanas

Huenda wewe ulikuwa ni moja kati ya watu waliokuwa wameshtushwa na taarifazilizokuwa zimeenea wiki mbili zilizopita kuwa Vanessa Mdee na Shilole wana bifu, ukweli umejulikana usiku wa May 29 2016, kuwa haikuwa bifu bali ni promo ya show yao ya pamoja waliofanya usiku huo.
3X6A9861
Dakika chache kabla ya Show Vanessa Mdee akiwa backstage alinukuliwa akisema “Kiukweli haukuwa ugomvi bali tulijaribu kuwaonesha watu kuwa usiamini kila unachokiona kwenye mitandao, namuheshimu sana Shilole katika kazi zake, lakini baada ya sisi kufanya vile watu walionekana kama wanataka kuona sisi tukigombana”
3X6A9862
3X6A9876
3X6A9878
3X6A9879
3X6A9893
3X6A9894
3X6A9897
3X6A9898
3X6A9906
Vanessa alimsurprise Shilole On Stage kwa kumletea zawadi ya ugali kwenye stage
3X6A9914
3X6A9915
3X6A9919

Alikiba Akanusha Kumuimbia Jokate Wimbo ‘Aje’

Alikiba amesema Aje si wimbo aliomuimbia Jokate wala msichana yeyote bali aliimba kwaajili ya mashabiki wake.
jo-e1434705782158
“Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu,” Kiba alikiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.
Hata hivyo Kiba alikiri kuwa kumtaja Wema kwenye wimbo huo kimekuwa ni kitu cha surprise kwa mrembo huyo.
Aje ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri kwa sasa si tu Tanzania, bali sehemu nyingi za Afrika.

Hizi Ndizo Ngoma Kali Za Mastaa Zilizohit Ambazo Raymond alishiriki kuziandika

Raymond ni msanii mwenye vipaji vingi vilivyomvutia Diamond amsainishe kwenye label yake, WCB.
13108612_1134282759961344_2144088758_n
Miongoni mwa vipaji alivyonavyo ni uandishi wa nyimbo huku akiwa ameshiriki kuandika hits kadhaa zikiwemo za bosi wake, Diamond. Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, Ray alisema bosi wake ni mtu anayependa sana kushauriana na watu mbalimbali ili kupata kitu kizuri na ndio maana alimpa nafasi kijana wake ampe melody na mistari kadhaa kwenye verse ya remix ya Zigo ya AY.
“Yeye ni msanii wa melody za kulalamika sana kwahiyo alivyosikia ile beat ina uchizi flani, kuna baadhi ya melody kama ile mukide mukide nikamuambia tukiweka hapa inakaaje, yeye anatafuta maneno,” alisema Ray.
Amesema pia alishiriki kutoa idea zake kwenye Make Me Sing. Lakini amedai kuwa bosi wake pia ameshiriki kumpa maneno mengi na melody kwenye wimbo wake Kwetu. Pia amedai kuwa Harmonize naye amechangia ideas zake kwenye wimbo wake Natafuta Kiki.
Kwa upande mwingine Ray alishirikiana an Dogo Janja kuandika wimbo wake My Life.
Akizungumzia boss wake, Ray amesema Diamond ni msanii anayeishi maisha simple kuliko watu wanavyoweza kudhani.
Msikilize zaidi hapo chini.

Download Audio: Mc Galaxy ft. Lybra - Summer Dance


Download New Video | Olamide ft. Wande Coal & Phyno - Who You Epp?




Download/Listen New Audio | Raymond - Freestyle

Kabla ya kumfahamu akiwa WCB, Raymond ni msanii wa rap aliyefahamika kitaa kwa uwezo wake mkubwa wa kufreestyle. Wengi hawaujui uwezo wako huo hivyo sasa tunakupa ladha ya uwezo wake huo kama alivyouonesha kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.
                                                                      DOWNLOAD
http://old.hulkshare.com/dl/vok3pftl8e0w/Raymond_-_Freestyle.mp3?d=1

Download New Audio | Chibu Wayaya Ft Fetty - Nahuhitaji

                                                                                                                                                                                     https://mkito.com/download/index?id=d446001193001fa4b1d29dd8e36868936963865e&title=Nakuhitaji&xid=11736&dt=f&cur=undefined&referrer=

Wizkid Apewa Shavu Na Chris Brown, Amuongeza Kwenye ‘One Hell of A Nite Tour’ Ulaya

Wizkid tayari anaishi ile ndoto ambayo wasanii wengi wa Afrika bado wanaiota. Kutoka kushirikishwa kwenye wimbo wa Drake ‘One Dance’ uliopo kwenye album Views na ulioshika namba moja kwenye chart za Billboard 100, hadi sasa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaomsindikiza Chris Brown kwenye ziara yake ya ‘One Hell of A Nite Tour’ barani Ulaya.
13248976_820765204721577_268213544_n
Taarifa hiyo ilitolewa na Chris Brown mwenyewe kwenye akaunti yake ya Instagram kabla ya Wizkid naye kuandika: 5th – 11th June I’ll be supporting my brother @chrisbrownofficial !! Get ur tickets!! #Onehellofanitetour Bringing the African wave!!”
Wizkid ana wimbo aliomshirikisha muimbaji huyo wa Marekani mwenye mashabiki wengi.

Madawa Ya Kulevya Yamenirudisha Nyuma, Hilo Liko Wazi – Ibra Da Hustler

Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, amewataka wasanii wenzake kukaa mbali na matumizi ya Madawa ya kulevya. Ibra Da Hustler
Rappa huyo ambaye alikaa rehab kwa muda mrefu ili kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, ameiambia Bongo5 kuwa matumizi ya Madawa ya kulevya yamesabisha apoteze dira ya maisha yake.
“Kusema kweli Madawa ya kulevya yamenirudisha nyuma sana, sitaki kuzungumza mengi nadhani hilo liko wazi,” alisema Ibra.
“Mimi sikuwa hivi, niweyumba sana, ndio maana napenda kusema kila kitu kwenye maisha kinatokea kwa sababu, na wenzangu wajifunze kupitia mimi, na kwa wale wenzangu ambao walikubwa na matatizo kama yangu,” aliongeza.
Ibra amesema kwa sasa ameacha kabisa matumizi ya Madawa ya kulevya huku akidai sasa hivi anatumia pombe na sigara tu.

Yasome Hapa : Mambo Matatu yanayoipa Nguvu Lebo ya Wasafi Kufika Mbali

Hutakiwi kushangaa siku ukisikia lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kuwa ipo juu zaidi ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, hiyo ni kutokada na mikakati pamoja na jitihada zinazozidi kuwekwa na uongozi wa lebo hiyo.

Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne akiwemo Diamond, Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na taarifa za chini chini kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa chini ya lebo hiyo huku bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na tayari amesharekodi wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika Kusini. Lakini pia nje ya kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya Diamond ni biashara kubwa ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa kila siku.

Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.

Ukubwa wa jina la Diamond

Hili halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho ni kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na kazi zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.

Mashabiki wanaomsupport Diamond

Diamond ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo tayari kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na maneno kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza kutumia pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya sasa kwa Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.

Menejimenti ya WCB

Uongozi wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa kufaulu kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya na hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza wakaifanya lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka kufika huko.

Source:Bongo5

Meneja wa Alikiba Afanunua Nini Kitakachokuwepo Kwenye Alikiba TV

Series ya taarifa kubwa za michongo ya kimataifa aliyopata Alikiba mwezi huu imeendelea.

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’

Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.

“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.

“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.

Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.

Baada ya Kutoboa Pua Sasa Diamond Aweka Meno ya Dhahabu...Mashabiki wake Waduwaa

Diamond Platnumz's Baby Mama, Zari shared a pic of her hubby, Diamond Platnumz to ask for the fans to vote for Diamond on BET 2016 Awards, On his Pic Diamond platnumz seems to make changes on his teeth, not yet known even he has attached 'golden teeth' or not and has made fake nose piercing again as few weeks did.

Diamond platnumz is in Dallas for his USA tour, when In Dallas he met with Kenyan Comedian Eric Omondi, See a short Video Diamond shared on his account with his Manager, Babu Tale and Eric Omondi.

Wolper Ambadilisha Jina Diamond Platnumz Na Kumuita Jina Hili

Kwa sasa headlines nyingi katika upande wa mastaa Tanzania ni stori kuhusu penzi la muigizaji Jackline Wolper na msanii wa Bongo fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) Harmonize ndio Topic kubwa town.

Katika mahojiano na Take One ya Clouds TV  na Zamaradi Mketema, Jackline Wolper ameeleza mambo kadhaa kuhusiana na penzi lake la Harmonize, Diamond ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake anachukuliaje mahusiano yao?

“Diamond rafiki yangu sana ni mtu ambae nategemea hata kuja kufanya nae filamu, Diamondi ni rafiki yangu sana licha ya watu wanaweza wasielewe, lakini sasa hivi Diamond ni baba mkwe wangu,

“kuhusu Harmonize nampenda kwa sababu ana hofu ya mungu, ana heshima sana mwisho hawezi kufanya maamuzi bila kuomba ushauri, katika kunipenda mimi alipiatia pia kuomba ushauri kwa Diamond ambaye ni boss wake kaka yake na kupewa ruhusa kwa hiyo Baraka zimetoka kwa Diamond mwenyewe”


-udakuspecially

Hatimaye Wema Sepetu Akubali Kuolewa Na Idris, Afunguka Zaidi Hapa....!

Penzi la Wema na Idriss kwa sasa linazidi kupamba moto, mpaka kupelekea Wema Sepetu kuanza kuwaza kufunga ndoa na Idriss. Wema alifunguka hayo katika video alipoulizwa na shabiki yake ni lini atafunga ndoa na Idriss.

Tuesday, May 24, 2016

Check Hapa | Video Ya Kinyambe Akijitabiria Kufa....

Watch New Video | Shery Zuu Ft Msaga Sumu – BABU UYO (Official Music Video)

Screen Shot 2016-05-25 at 12.02.18 AM

Harmonize Atoa Maneno Ya Kejeli Kwa Wema Sepetu, Bifu Zito Latabiriwa..... Angalia Video Nzima Hapa....

Mzazi Mwenza Wa Aslay Afunguka Kuhusu Mahusiano Yao

Download Audio: Young Killer Ft. Mr Blue - Kumekucha




                                    

Je ni Kweli Supu ya Pweza Inaongeza Nguvu za Kiume? Ukweli Huu Hapa

HAMU ya tendo la ndoa kwa mwanadamu au mwanamke ni moja ya hisia za msingi kwa mtu wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi.

Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili.

Panapokuwa na changamoto Fulani, wajasiriamali huiona changamoto hiyo kama fursa, na fursa hiyo imeonekana kuwanufaisha vijana wanaokaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la kimataifa la magogoni baada ya supu ya samaki huyo aina ya pweza kuonekana kupendelewa sana na wanaume wa rika zote nchini.

Lakini siku za hivi karibuni hiki kitumbua kimonekana kuingia mchanga, yaani biashara kuharibika baada ya uvumi kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba wakaanga samaki wanaweka dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya viangra ili kuisisimua miili ya wateja wao,

Ni imani ya wanaume wengi wa pwani na hata kutoka bara ambao huishi ukanda wa pwani siku hizi hupenda supu ya pweza kutokana na wingi wake wa virutubisho ambavyo huamini kuwa vinaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.

Baadhi ya vijana waliozungumza na  wamedai kwamba mara nyingi wanatumia supu ya pweza ili kusisimua mwili huku wengine wakidai wanatumia kama kiburudishotu sio kama dawa ya kuongeza nguvu.

ULAJI wa supu ya pweza, kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na chakula hicho.

Kwa siku za hivi karibuni vijana wengi wameonekana kuchangamkia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume bila kushauriwa na daktari

Lady Jaydee Haikufaa Uimbe Uliyoimba Ndani ya Wimbo wa Ndindindi

Nijikite Madani.

Bila Shaka watu wengi humu tuna mkubali sana mwanamziki Huyu nguli wa miondoko ya r n b ndani ya bongofleva. Huyu Ni kati ya wasanii wakubwa waliofungua uhusiano mzuri wa kimziki baina ya Tanzania Na Afrika kusini ref; Njalo! Hata kuna video Jide aliwahi kufanya Kule bondeni, kufuatia harakati zake Leo hii wasanii wengi wakubwa wanaowika Miaka hii wanafuata Nyayo zake Na kujaribu kupanua wigo wao wa mashabiki barani Africa Na duniani Kwa ujumla kupitia mlango uliofunguliwa Na Jide huko SA.

Wote tunafahamu mahusiano Na Ndoa aliyopitia dada yetu Huyu kipenzi. Tunajua changamoto kubwa aliyokabili katika Ndoa Yake ambayo Kwa kiasi kikubwa ilikua inampact KUBWA tu kimafanikio Yake ya kimziki .

Ni Kweli huenda Shemeji yetu (G) amemkosea Mara nyingi dada yetu Ila Kwa maoni yangu Mimi bado Naona alikua Na mchango Mkubwa sana Kwa dada yetu( sijasema Jide hawezi kusimama kimziki bila G) Ila nafikiri haikua vema kumuimba mtaliki wake katika wimbo huo!

Ikumbukwe G alivumilia maneno mengi sana kuhusu hali ya Huyu dada yetu! Hata zaidi G mwenyewe sio mtu wa visasi Na majibizano! Amekua cool sana kuzungumzia mahusiano Na hali Yao ya mahusiano Yaani Kwa kifupi Jamaa ameonyesha Kifua cha kiume Na Heshima Kwa aliekua mkewake.

Jide anamashabiki wengi sana, Yaani hata angeimba chochote bado ngoma Yake Ingelizwa sana tu! Hata angetaka kuimba kipaji chake Kua kimejaa Ndindindi bado ingefaa tu. Ukiangalia umri wake Na jinsi amejijengea heshima Kwa mashabiki Na maadui zake ilifaa aonyeshe ukomavu Kwa ku'move on bila kuzungumzia lolote kuhusu Ndoa vunjifu!

Mwisho Kabisa ili tuendelee kukuheshimu Kama Sasa dada yetu kipenzi Tunaomba usizungumze lolote kuhusu G, wewe simama kivyako tu, sote tunajua uliyopitia ingawa kiundani zaidi unajua mwenyewe, Na huenda unaimba Ili kupunguza machungu Ila jikaze, kumbuka wewe Ni Komando! Muache brother aendelee tu Na Maisha Yake, Hebu ona hata Hakumzuia Dina kufanya interview Na wewe ingawa Na uhakika angetaka angezuia tu!

IMBA TUCHEZE!!

Icheki Hapa Ndege Inayotumia Umeme Imetengenezwa Kwa Ajili Ya Matumizi Ya Nyumbani

Nchini Ujerumani wametengeneza Ndege aina ya LILIUM  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yenye siti mbili, shepu ya yai na inatumia umeme, imetengenezwa na  mainjinia wanne wakijerumani wakidai kuwa ndege hiyo yenye kupunguza matumizi na kurahisisha usafiri kwa watu.
Ndege hii inasemekana kuwa na uwezo wa kwenda hadi spidi ya kilometa 400 kwa saa, kutumika  kwenye eneo tambarare, kupaa na kutua kwa mita 15. Kingine kikubwa ni kwamba inatumia umeme na inachajiwa kama simu pia haina kelele pia ni kwa ajili matumizi ya mchana tu kwenye hali ya hewa tulivu na sio usiku.
Mmoja wa msaidizi wa mmiliki wa ndege hiyo, Daniel weigand amesema wana mpango wa kuiingiza sokoni mwaka 2018, ameyazungumza haya …………
>>>”tunataka ndege isiyo na gharama kubwa wala isiyokuwa na tatizo la utumiaji wa miundombinu yake, pia iweze kutumika na watu wengi wenye uwezo wowote ule sio watu wenye uwezo mkubwa tu ndo waweze kununua ndege hii”.
lilium1
lilium2


lilum5 lilium3
MillardAyo.Com

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.