Wednesday, June 1, 2016
Mzee Majuto Akanusha Uvumi Unaoenea Ya Kwamba Amestaafu Uigizaji..!
Msanii wa filamu za kuchekesha, King Majuto amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kwamba amestaafu kuigiza.
Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatano hii, Mzee Majuto amedai sio kweli kwamba amestaafu kuigiza ila kuna baadhi ya filamu ambazo hatafanya tena.
“Watu wameniwekea maneno mdomoni, sijasema nimeacha kuigiza,” alisema Majuto.“Wakati nipo Hija mwaka jana nilikuwa nafikiria niache kabisa kuigiza, lakini baada ya kurudi nikaona nalazimika kuendelea kuigiza ili nipate pesa za kuendesha maisha yangu, kwa sababu bila filamu nitakufa njaa,”
Pia muigizaji huyo amesema hafanyi tena stand up comedy kwa kuwa wakati anafanya kuna matukio ambayo yatakuwa yanaendelea katika ukumbi ambayo dini yake hayaruhusiwi.
Pia Majuto amewataka mashabiki wa filamu zake kuendelea kusubiria kazi zake ambazo atakuwa anaandaa mwenyewe.
Labels:
Entertainment,
Mzee Majuto
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment