Diamond
Platnumz hana mpango wa kuwa chini na record label yoyote duniani.
Infact hitmaker huyo amedai kuwa makampuni kibao yamewahi kummendea
yakitaka awe chini yake lakini akayapiga kibuti.
“Mimi
nimeshaapprochiwa na makampuni mengi sana kutaka kunisaini, mengi sana,
mengi hata wanayoyasikia, mengine wanayasikia,” Diamond ameiambia 255
kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Lakini
nafikiria kwamba unapotaka kunisaini mimi unataka kunifanyia nini? Una
kitu gani cha kunioffer cha kuona mimi unisaini? Video? Mimi naweza
kufanya video zangu hadi za wasanii wangu. Collabo? Collabo mimi naombwa
napigiwa simu, msanii wa Marekani wa Tanzania, yeyote nikitaka kufanya
chochote naweza kufanya naye,” ameongeza.
“At
the end of the day is all about money, nina capital, nina network, ndio
maana nikasema kwa nilipofikia sio nibaki mimi tu, niwe na record label
yangu. So sifikirii kusainishwa, nafikiria kusaini watu ili kuweza
kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.”
“Kwa
mfano unataka kunisaini, unataka kunifanyia nini? Nikaperform mbinguni?
Tuzo zote ambazo mwaafrika anatakani kuziwin.. sijawahi kupata BET na
Grammy tu, nataka nipige na Grammy nioneshe kabisa napiga na Grammy.
Ukiniambia nasainiwa it doesn’t make sense. Naamini management yangu ni
kubwa kuliko mtu yeyote akinisaini, akisema anifanyie promotion hatoweza
kufanya promotion ninayoifanya mimi,” amesisitiza.
Diamond
aliyeanzisha record label yake, WCB tayari amewasaini Harmonize na
Raymond huku kukiwa na uwezekano kuwa amemshamsaini Rich Mavoko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment