Baada ya kambi ya WCB kuonekana wasanii wake wanapenda kutoka
kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, uongozi wa kambi hiyo
umelizungumzia swala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii, Mmoja kati ya
viongozi wa juu wa kambi hiyo, Babu Tale, amesema ni bahati kwa wasanii
wake kupata wanawake waliowazidi umri.
“Sisi tunameneji wasanii hatumeneji hisia zao, lakini ikitokea msanii
fulani amempenda mwanamke fulani tunamuacha kwa sababu ni mapenzi
yake,” alisema Tale. “Tunaona ni bahati kwa wasanii wetu kupata wanawake
waliowazidi umri, hiyo ni bahati (anacheka) kwa sababu wanamuenzi Mtume
Muhammad (s.a.w.w.) alimuoa Bi Khadija ambaye alimzidi umri,”
Hata hivyo, Tale alisema ndani ya WCB hawameneji mapenzi bali wanammeneji msanii pamoja na kazi zake.
Saturday, June 4, 2016
Babu Tale: Wasanii Wa ‘WCB’ Wana Nyota Ya Kupata Wanawake Wenye Umri Mkubwa Zaidi yao (Video)
Labels:
Babu Tale,
Entertainment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment