Saturday, June 4, 2016

Irene Uwoya kuja na tamthilia yake mpya iitwayo ‘Drama Queen’

Mwigizaji wa filamu, Irene Uwoya baada ya ukimya wa muda mrefu bila kuachia kazi, anajipanga kuachia tamthilia yake mpya iitwayo ‘Drama Queen’.
Irene Uwoya
Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Uwoya amesema tamthilia kwa sasa zinalipa vizuri kutokana na runinga nyingi kuhitaji tamthilia.
“Nataka kufanya tamthilia ambayo inaitwa Drama Queen,” alisema Uwoya “Mimi ndio Drama Queen mwenyewe, na niliamua tu kufanya kitu tofauti ili kuleta ushindani katika game.”
Katika hatua nyingine, Irene Uwoya amewataka mashabiki wake kusubiria kazi zake mpya za filamu ambazo atazitangaza hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.