Saturday, June 4, 2016

Pichaz : Shetta Akitambulisha Menejimenti Yake Pamoja Na Kuwashukuru Mashabiki



Mali wa Muziki wa Bongo Fleva, Shetta a.k.a Nurdin  Alhamisi hii aliandaa sherehe maalum ya kuwashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kumfikisha hapo alipo pamoja na kuitambulisha management yake mpya.
4K0A8344
Shetta akimtambulisha baunsa wake, anaitwa Mbrazili

Sherehe hiyo ambayo iliambatana na uzinduzi wa management ya Shetta, ilipambwa na mastaa mbalimbali wa muziki, filamu pamoja na wadau wa sanaa ya muziki.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Rouge Hyatt Recency Hotel, Jijini Dar es salaam, Shetta alisema ameamua kufanya hivyo ili kuwashukuru wadau mbalimbali waliomsaidia kumfikisha hapo alipo.

“Kusema kweli Shetta amekuwa na safari ndefu katika maisha yake ya muziki, lakini haya mafanikio yamekuja kwa michango ya watu wengi sana, media, mashabiki pamoja watu wangu wa karibu. Kwa hiyo nimeona bora niwaite hapa ili tujipongeze kwa hapa tulipofikia, kwa sababu haikuwa kazi rahisi. Hapa nimewaalika watu mbalimbali pamoja na mashabiki wangu ili waje na wao kufurahia hapa nilipofikia, kwa hiyo tutakumwa na kula pamoja,” alisema Shetta.

Pia Shetta aliweza kutambulisha management yake mpya, baunsa wa kumlinda pamoja na dancer. Angalia picha.
4K0A8272 4K0A8320 4K0A8328 4K0A8338 4K0A8346 4K0A8351 4K0A8363 4K0A8316 4K0A8310 4K0A8307 4K0A8292 4K0A8280 4K0A8277 4K0A8261 4K0A8255 4K0A8244 4K0A8266
CC:HARAKATIZABONGO

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.