Kwa mujibu wa data za robo ya mwisho ya mwaka 2015 na robo ya kwanza ya mwaka 2016 kutoka kwenye kampuni ya utafiti wa vyombo vya habari Geo Poll yenye makao yake nchini Marekani, kituo hicho kilichukua asilimia 20 ya watazamaji (audience share) katika miezi minne ya mwisho (October – December) ya mwaka 2015 na kushuka kwa 2% katika kipindi cha miezi minne ya kwanza ya mwaka 2016 (January – April), kwa kuwa na asilimia 18.
Clouds TV imeendelea kufanya vizuri pia kwa kukamata nafasi ya pili kwa kuwa na 17% katika robo ya nne ya mwaka jana huku ikipanda kwa 2% katika robo ya kwanza mwaka 2016 hadi kufikisha 19%.
Ripoti hiyo imeonesha pia kuwa EATV imefanya vizuri katika robo ya kwanza mwaka huu kwa kuwa na 16%.
Vituo vilivyofuata ni pamoja na TBC 1, Star TV, Channel 10, TV1, TBC 2. Vingine vikiwemo Azam TV, Mlimani TV, Capital TV na vingine vimeonekana kufanya vibaya kwa kugawana 1% tu iliyosalia, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Kwa upande wa ratings, East Africa TV na TV1 ziliongeza katika robo ya kwanza huku ITV ikipoteza ratings kwa kiwango kikubwa. “TBC1 and Channel 10 have also dropped in their ratings in Q1,” inasema ripoti hiyo.
RADIO
Kwa upande wa vituo vya redio, Clouds FM bado imeendelea kuwa kinara kwa kuvuta 28% ya wasikilizaji katika robo ya mwisho 2015 huku ikipoteza 2% katika robo ya kwanza mwaka huu na kuwa na 26%.
TBC Taifa imeonesha kufanya vizuri kwenye robo ya kwanza mwaka huu kwa kuwa na 13% ikifuatiwa na Radio Free Africa iliyong’ang’ania kwenye 10% huku Radio One na TBC FM zikifuatia. Habari njema kwa EFM ambayo hadi sasa bado inasikika Dar es Salaam na Pwani pekee ambayo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa na wastanii wa 5.5% mbele ya East Africa Radio, Times FM na Capital FM.
No comments:
Post a Comment