Baada ya mashabiki na wadau mbalimbali kujadili kauli ya Wema Sepetu ya
kwamba anatumia Tsh 4.8 kwa ajili ya nywele zake kwa mwezi mmoja, mpenzi
wake Idris Sultan amesema matumizi hayo yanaendana na hadhi ya mrembo
huyo.
Aidha katika kauli nyingine ambayo Wema aliitoa mapema mwaka huu,
alisema anatumia Sh 30,000 kwa ajili ya chakula kwa siku na kama
atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Idris Sultan ambaye ni mshindi wa shindano
la Big Brother 2014, amesema haoni tatizo kwa mpenzi wake huyo kuwa
namataumizi makubwa kwa kuwa yeye mwenyewe ni mtafutaji.
“Kwa level yake anafaa, kila mtu na level yake,” alisema Idris. “Kwa
hiyo nina maanisha kila mtu ana thamani yake, na kila siku hadhi ya
maisha yake inapanda na pia anafanya kazi ndiyo maana anafikia katika
level hiyo,”
Pia Idris alisema watu wanatakiwa kutambua kwamba jinsi uchumi wa mtu
binafsi unavyokuwa basi pia na maisha yake hudabilika pamoja na
muonekano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment