Mfalme wa bling bling nchini Kenya, Prezzo amedai kuwa bondia tajiri wa Marekani, Floyd ‘Money’ Mayweather ni mshkaji wake na huwa wanapiga story za hapa na pale.
“Mimi nina connection, mimi na Floyd Mayweather yule bondia mimi na yeye tunaongeaga yaani,” Prezzo alikiambia kipindi cha Funiko Base cha Radio 5 ya Arusha.
“Fight yake sio ile iliyopita, ya mwisho, ile fight yake ya 48 alikuwa amenialika shida ilitokea kwamba nilikuwa sijarenew visa yangu ya America na huwa kuna bonge la foleni, so siku yeyote nikienda Las Vegas usishangae kuniona mimi na Mayweather tunakamua yaani full makamuzi na tena kwa mara nyingine hiyo ndio tofauti yangu na huyo jamaa anaitwaje tena?” alijitapa rapper huyo.
Msikilize hapo chini.
No comments:
Post a Comment