Monday, June 6, 2016

Harmonize Amnunulia Wolper Gauni La Tsh Milioni 1

IMEVUJA ! ‘Kinda’ wa Bongo Fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ ambaye anatamba na kibao chake cha Bado, anadaiwa kumnunulia mpenzi wake, staa wa filamu, Jacqueline Walper ‘Wolper’ gauni lenye thamani ya shilingi milioni moja.
Chanzo kilicho karibu na msanii huyo wa lebo ya WCB, kinadai muigizaji huyo ni mwanamke wa gharama, ambaye mavazi na maisha yake, yanahitaji mtu mwenye uwezo kifedha, lakini kwa kijana huyo mwenyeji wa Mtwara ni kama anajiumiza.
“Yaani hivi karibuni wakati akienda kumtambulisha kwao, alilazimika kumnunulia gauni la shilingi milioni moja wakati yeye mwenyewe anavaa mavazi ya kawaida tu kama wasanii wenzake, hapa kweli mapenzi yamekubali,” kilisema chanzo hicho, kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Wolper na kumsomea tuhuma hizo, lakini alicheka na kudai hana la kusema kwa vile maisha ya kimapenzi na msanii huyo ni ya kawaida tu.
Harmonize mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema kwa wakati huo hakuwa katika eneo zuri, akiahidi kupiga yeye mwenyewe kwa gazeti hili baadaye lakini hadi linakwenda mitamboni, hakuwa amepiga.
Kwa upande wa meneja wa msanii huyo, Mohamed Salum ‘Rikadomomo’ alisema anamsimamia kimuziki tu, maisha yake binafsi hayamhusu.
-GPL

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.