Thursday, June 30, 2016

Ajabu: Mwanaume Afunga Ndoa na ‘Simu Yake’ Kanisani

ndoa na simu
Mwanaume mmoja aliyejitambusha kwa jina la Aaron Chervenak mwenye umri wa miaka 34 na mkazi wa Los Angeles nchini Marekani, amefanya tukio la aina yake baada ya kufunga ndoa kanisani na simu yake ya kupapasa (smartphone).
Ndoa ya simu 2
Mwanaume huyo alisafiri hadi Vegas kulisaka kanisa moja ambalo lilimkubalia kufunga ndoa na simu yake na kula kiapo kama ambavyo alipaswa kula kiapo kwa mrembo aliyeyagusa maisha yake na kuamua kumfanya mkewe wa maisha.
Akizungumzia sababu zilizopelekea yeye kufanya tukio hilo, kupitia makala maalum ya ndoa yake hiyo, Aaron alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu ya ukweli kwamba simu zimekuwa zikichukua nafasi kubwa ya mapenzi na uhusiano na zikifanya jukumu kubwa la kuwatuliza watu katika dunia hii.
“Kama tutakuwa wakweli, tunaunganishwa na simu katika viwango vingi vya hisia. Tunaikimbilia kututuliza, kutulaza usingizi, kuweka unafuu kwenye mawazo yetu. Na kwangu, huo ndio uhusiano nilionao na simu yangu hii,” alisema Aaron.
Ndoa ya simu 3
“Kwa mantiki hiyo, simu yangu hii imekuwa na uhusiano wa muda mrefu na mimi na ndio maana nimeamua kufunga nayo ndoa,” aliongeza.
Kuhusu jinsi alivyokubaliwa kufanya tukio hilo kanisani, alisema kuwa alijaribu kuwasiliana na uongozi wa kanisa hilo kuona kama angeruhusiwa lakini alihakikishiwa kuwa anakaribishwa kwa mikono miwili.

Share na Marafiki: 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname

Powered by Blogger.