Friday, June 17, 2016
Mwasiti kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha Chidi Benz
Kama umemiss sauti ya Chidi Benz, kuna habari njema.
Mwasiti anatarajia kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha rapper huyo. Amesema huo ni wimbo waliofanya kitambo lakini ulikuwa bado kwenye makabati.
Akiongea na 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Mwasiti amesema wimbo huo uliorekodiwa miaka miwili iliyopita unaitwa ‘Wanipa Raha’ na kwamba ni bonge la ngoma. “Ni kazi nzuri ambayo huwezi kusema imerekodiwa miaka miwili au mitatu iliyopita utasema ni ngoma ambayo imerekodiwa jana labda kwasababu ni kazi nzuri sana,” amesema Mwasiti.
Amesema wimbo huo umetayarishwa na Tudd Thomas.
Mashabiki wengi wameimiss sauti ya Chidi ambaye hivi karibuni alipelekewa Bagamoyo kwenye kituo cha kusaidiwa waathirika wa madawa ya kulevya.
Ametoka na wiki hii ameonekana kwenye picha mpya akiwa ameanza kurejea kwenye afya yake.
Labels:
Entertainment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment