Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Joachim Kimaryo ‘Master Jay’,
ameweka wazi mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu,
Sara Kaisi ‘Shaa’.
Master J amesema Shaa atakuwa mke bora kwake kwani tayari ameshaishi naye kwa miaka 10 bila matatizo yoyote.
“Miaka 10 niliyoishi naye nimemwelewa vizuri, anastahili kabisa
kuitwa mke wa Master J hapa nafanya taratibu za kumuoa ili tuishi maisha
ya mke na mume,” Master J aliliambia gazeti la Mtanzania.
Mtayarishaji huyo wa muziki alisema kwamba anampenda Shaa kwa sababu
ni msichana anayejielewa, licha ya kuwa msanii hasahau jamii
inayomzunguka huku akijituma sana katika kazi zake zote kwa ujumla
Wednesday, June 15, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment