Muimbaji huyo ambaye pia anamiliki, studio ya picha pamoja na studio ya muziki ‘Wasafi Record’, aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa kila anachokipata anagawana na team yake.
“Tunashukuru mungu kile tunachokipata tunagawana na wengine, mpaka sasa tayari WCB imeajiri watu 42, hii ni hatua kubwa sana katika tasnia ya muziki wetu,” alisema Diamond.Katika hatua nyingine, Diamond amesema ni swala la kiungwana kulipa kodi katika kile anachopita.
“Unajua katika kila penye biashara ni lazima na ni haki kulipa kodi ili pato la taifa liingie, namna ya mapato maana yake nini, serikali inatambua kazi na inailinda. So serikali ipo na inafanya hivyo, lakini labda kuna nyanja nyingine hawazioni, kwa hiyo sisi kama tunataka kazi zetu zichangie pato la serikali, lazima tuwe mstari wa mbele katika kuonyesha nyanja zote za mapato, kwamba tunafanya hichi na hichi, ridhiki zetu zinatokea hapa na hapa, mishahara yetu tunagawa hivi na hivi, na kama serikali inavyoagiza katika kiasi hichi tunatakiwa kutoa kiasi hichi kwa ajili ya serikali. Kwa hiyo tusilalamike tu serikali haifanyi kazi wakati sisi tunaweza kuwa wa kwanza kuirahisishia serikali kutekeleza majukumu yake,” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment